Ali Kiba Adai Alianza Kuonyesha Anapenda Muziki Tangu Akiwa na Siku 7 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ali Kiba Adai Alianza Kuonyesha Anapenda Muziki Tangu Akiwa na Siku 7

Bet Sasa
Staa wa muziki Ali Kiba amesema wazazi wake walikiona kipaji chake cha muziki toka akiwa mchanga.
Akiongea na Chill na Sky hivi karibuni, Kiba amesema aliambiwa alianza kucheza muziki akiwa na siku saba.

“Unajua mimi zamani kidogo wakati nazaliwa, nimeanza kucheza muziki nikiwa na siku saba. Nimeambiwa nilikuwa nikisikia muziki nacheza, mimi kitanda changu baba yangu alininunulia kutoka Nairobi, kilikuwa kina radio, lazima waweke station ambayo inapiga muziki hapo ndio naweza kulala, ikizimwa nalia,” alisema Ali Kiba.

Aliongeza, “Kwa hiyo nilikuwa mpenzi wa muziki kutoka kipindi hicho na mpira ukaja baadae, nikawa nacheza nyumbani, shuleni baadae nikawa vizuri kabisa,”.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.