AJABU: Nywele za Msanii Zauzwa Dola 35,000 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

AJABU: Nywele za Msanii Zauzwa Dola 35,000

Mjini kila kitu kina thamani yaani ukikihitaji lazima utoe hela, sikia hii, Shungi la nywele ya msanii nguli wa muziki chapa Rock na muanzilishi wa kundi la ”The Beatles” John Lennon aliyeaga dunia miaka 36 iliyopita imeuzwa kwa dola elfu thelathini na tano ($ 35,000) katika mnada mmoja huko Marekani
Kinyozi wa Muimbaji huyo maarufu kote duniani alificha shungi la nywele baada ya kumnyoa msanii huyo alipokuwa akijiandaa kuigiza katika filamu moja.Lennon aliuuawa mwaka wa 1980 mjini New York Marekani.
Mnunuzi mmoja shabiki sugu wa Lennon kutoka Uingereza ndiye aliyeandika hundi hiyo ya dola ($ 35,000).
Bidhaa zingine zilizotumika na kundi hilo la muziki la ”The Beatles”pia ziliuzwa katika mnada huo huko Texas.

Baadhi ya bidhaa hiyo ilikuwa nakala maalum ya albamu yao ya ‘Yesterday and Today’, iliyouzwa kwa dola laki moja u nusu ($150,000).

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.