Video na Picha: Shilole aingia studio Afrika Kusini kurekodi ngoma na producer wa Uhuru - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video na Picha: Shilole aingia studio Afrika Kusini kurekodi ngoma na producer wa Uhuru

post-feature-image
Shilole a.k.a Shishi baby anaendelea kufanya maandalizi ya kuupeleka muziki wake kimataifa, kwa kufanya kazi na watayarishaji wa muziki wa nje ya Tanzania.
Baada ya kufanya wimbo na producer wa Nigeria, Selebobo mwishoni mwa mwaka jana alipoenda nchini humo, Shishi ameingia studio kurekodi wimbo mwingine na producer wa Afrika Kusini, Dj Maphorisa wa kundi la Uhuru.
Me n my baddest producer in Africa about to do magic in the studio please follow him @djmaphorisa” ameandika Shilole ambaye yuko Afrika Kusini na Linah.
Maphorisa ameshafanya kazi na wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika akiwemo Wizkid, Davido, RunTown na wengine.
Baadhi ya wasanii wa Tanzania ambao tayari wamefanya kazi na producer huyo ni pamoja na Chege (Sweety Sweety) na Linah (Ole Themba).

-tubongetz

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.