Tigo Yapigwa Faini Kwa Uzembe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tigo Yapigwa Faini Kwa Uzembe

????????????????????????????????????
Meneja Mkuu wa Tigo, Deigo Gutierrez
KAMPUNI ya MIC Tanzania Limited (Tigo) chini ya mkurugenzi wake, Diego Gutierrez imepigwa faini ya Sh. Milioni 25 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kosa la kushindwa kudhibiti utumaji wa ujumbe wa ulaghai na udanganyifu kwa wateja wake.
Taarifa ya faini hiyo ilitolewa hivi karibuni jijini Dar na Mkurugenzi wa TCRA, Dk. Ally Simba ambapo alisema kampuni hiyo na makampuni mengine ya simu, yameshindwa kudhibiti utumaji wa ujumbe wa udanganyifu na kuwalaghai wateja.
Taarifa hiyo ilizidi kueleza kuwa, Tigo inapaswa kulipa faini ya Sh. Milioni 25 ambapo amri hiyo imetolewa hadi Januari 29, 2016 na endapo hawatafanya hivyo, mamlaka hiyo itachukua hatua za kisheria na kuidhibiti kampuni hiyo.
Mbali na ulaghai huo wa kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS), Novemba 8, mwaka huu Tigo ililalamikiwa na wateja wake kwa kutokuwa hewani siku nzima kitu ambacho kiliwasababishia wateja hao kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo kwa kukosa mawasiliano.
“Hawa Tigo hawapo makini kabisa. Haiwezekani kwa watu makini mtandao ukosekane siku nzima,” alilalamika mmoja wa watumiaji wa mtandao huo.
Mbali na hilo, watumiaji mbalimbali wa mtandao huo wamekuwa wakiulalamikia kwa kutoa huduma hafifu licha ya kujitangaza kuwa wapo vizuri.
“Kuna wakati wewe wa Tigo unampigia wa Tigo mwenzako, hapatikani! Ukirudia unampata na anakwambia hajazima simu. Huu ni uzembe mwingine wa mtandao. Lakini pia inaweza kuleta balaa zaidi ya wanavyofikiria wao Tigo,” alisema John, mkazi wa Dar.
Mbali na Tigo, makampuni mengine yaliyopigwa faini kwa kosa la kushindwa kudhibiti ujumbe wa udanganyifu na ulaghai kwa wateja ni pamoja na Benson Informatics Limited (Smart), Airtel Tanzania Limited Viettel Tanzania Limited (Halotel) na Zanzibar Telecom Limited (Zantel).

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.