Tazama Jinsi Msanii Prezzo Alivyotia aibu ‘LIVE’ kwenye Runinga ya KTN Kenya ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tazama Jinsi Msanii Prezzo Alivyotia aibu ‘LIVE’ kwenye Runinga ya KTN Kenya !

Moja ya story za burudani zilizochukua headlines weekend iliyopita Kenya, ni pamoja na ile inayomhusu Prezzo ambaye alifanya vitendo vya aibu kwenye runinga ya taifa na kuwashangaza wengi.
Prezzo KTN
Ijumaa iliyopita, CMB Prezzo alialikwa kwenye studio za KTN kwaajili ya mahojiano kwenye kipengele cha ‘Friday Briefing’ ambacho msanii anayealikwa hupewa nafasi ya kusoma taarifa ya habari.
Katika mahojiano na mtangazaji wa kituo hicho Betty Kyalo, Prezzo alionekana kama mtu ambaye hayuko sawa, aliyelewa au asiyejielewa kutokana na vitendo vya aibu na vya kitoto alivyokuwa akivifanya na kuonekana moja kwa moja (live) kwenye runinga.
Moja ya vitendo hivyo ni kama kumsifia mtangazaji huyo ambaye ni mke wa mtu kama vile hawako kwenye TV, kama “hiyo nguo imekupendeza, mume wako atakuwa mwenye bahati kuwa na wewe.”
Prezzo KTN2
Pia mwanzoni kabisa mwa mahojiano Prezzo alisimama na kumkumbatia ghafla kiasi cha kumkosesha kujiamini mtangazaji huyo, na wakati mwingine alikuwa akimkosea heshima kwa kumshika mara kwa mara kiasi cha kumsababisha mtangazaji huyo mrembo na aliyeumbika kisawa sawa akose pozi.
Majibu ya Prezzo yalikuwa kama mtu ambaye hajielewi, kuna muda alisema kuwa Beyonce wa Jay Z aliwahi kuwa mpenzi wake!!
Betty Kyalo alijitahidi kutopanic na kumdhibiti lakini kuna muda alionekana kukaribia kumshindwa.
Wakenya wengi wamemshambulia Prezzo kwenye mitandao ya kijamii na kusema kuwa hiyo ilikuwa moja ya interview mbaya kuwahi kufanywa na TV za Kenya.
Hata hivyo mtangazaji huyo kupitia Facebook ameandika kuwa mama mzazi wa Prezzo alimpigia simu kumuomba radhi yeye pamoja na watazamaji wa KTN kwa tabia mbaya aliyoionesha mwanaye.
“Just received a call from Prezzos mother, she is so remorseful over his behavior on #FridayBriefing and asks that KTN viewers forgive him.Prezzos mum says it was a pain watching her son embarrass himself on live tv and the family is currently in talks with him over it.” aliandika Betty Kyalo.
Jionee mwenyewe mahojiano hayo ya Prezzo na Betty Kyalo kupitia KTN:

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.