Shilole: Msisikilize Uzushi, Kama Nikipata Mpenzi Mpya Nitasema Mwenyewe ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole: Msisikilize Uzushi, Kama Nikipata Mpenzi Mpya Nitasema Mwenyewe !

Shilole a.k.a Shishi Baby amesema baada ya kuachana na Nuh Mziwanda bado jimbo la moyo wake halijapata mgombea mpya wa kuziba nafasi yake.
shishiz
Zimekuwepo tetesi kuwa Shishi anatoka na msanii mwingine wa Bongo fleva, Nyauloso zamani Bonge la nyau, huku wengine wakisema kuwa ana uhusiano na msanii wa Uganda, Eddy Kenzo.
“Mimi sijapata mpenzi mpya mimi nipo tu, mpenzi mpya nitasema mwenyewe kwa mdomo wangu mimi,” Shishi ameeleza kupitia 255 ya XXL. “ nifanye interview niseme jamani sasa nina mpenzi mpya, lakini saizi msisikie rumors zinazotokea subirini mimi niwahakikishie.” Alisema Shishi.
Kuhusu Eddy Kenzo Shishi amedai kuwa ni kama kaka yake lakini wanawasiliana sana, na kuongeza kama endapo urafiki wao utazaa penzi basi atatangaza rasmi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.