Real Madrid Walimtaka Mourinho Akawatosa ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Real Madrid Walimtaka Mourinho Akawatosa !

José Mourinho
Imedaiwa kuwa Read Madrid walimpa ofa Jose Mourinho ili arejee tena Santiago Bernabeu.
Rais wa zamani wa Real Madrid, Ramon Calderon ameiambia Sky Sports kuwa rais wa sasa Florentino Perez alimtaka Mourinho arejee kwenye klabu hiyo kabla ya kuamua kumpa Zinedine Zidane baada ya kumtimua Rafael Benitez.
“Nadhani sio siri kuwa rais wa sasa alimpenda sana Jose Mourinho na Perez aliwasiliana naye kabla ya kuamua kumchukua Zidane,” alisema Calderon.
“Inavyoonekana, Mourinho hakupenda kuja kipindi hiki cha msimu na Zidane alikuwa hapa kwahiyo itabidi tusubiri kuona nini kitatokea wiki chache zijazo.”
Manchester United pia wamedaiwa kuwa na nia ya kumchukua kocha huyo aliyetimuliwa na Chelsea.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.