Rapper Joh Makini kuzifanyia video ngoma zake za zamani ‘Nikumbatie’ na ‘Kilimanjaro’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rapper Joh Makini kuzifanyia video ngoma zake za zamani ‘Nikumbatie’ na ‘Kilimanjaro’

Bet Sasa
post-feature-image
Rapper wa kundi la Weusi, Joh Makini amesema anataka kufanya video mbili za nyimbo zake za mazani, Kilimanjaro aliyomshirikisha Lady Jaydee na Nikumbatie aliyofanywa na Fundi Samweli kwa kuwa anaamini nyimbo hizo zinaweza kufanya vizuri zaidi kimataifa.

Rapper huyo aliyeachia Don’t Bother miezi kadhaa iliyopita, amekiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV kuwa ana imani kazi hizo zinaweza kwenda mbali zaidi.

Sina kitu ambacho nimekosa katika video zilizopita labda quality ambazo zinapatikana sasa hivi kama ningezipata wakati ule video zingeenda mbali zaidi,” alisema.

Sina mpango wa kurudia video ya wimbo wowote lakini na mpango wa kufanya video za nyimbo zangu ambazo hazikupata video, Nikumbatie na Kilimanjaro, ni ngoma ambazo nahisi zilistahili kuwa na video kwa sababu ni nyimbo ambazo naona zikipata video zitaenda mbali zaidi. Pia standard ya video zangu nataka iwe inaenda mbele, kwahiyo watu wategemee kazi nzuri.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.