Picha za ndoa FEKI ya Linex zampa Presha Mama yake. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha za ndoa FEKI ya Linex zampa Presha Mama yake.

Linex hakuwashtua mashabiki wake tu kwa picha za harusi kwenye Instagram bali pia mama yake.
Hata hivyo Linex amedai mama yake alipata mshtuko wa furaha baada ya kuamini kuwa hizo ni dalili za mwanae kuja kuoa siku moja.
“Hizi picha tukio linaweza kutokea kweli,” alikiambia kipindi cha E-News cha East Africa Television.
“Hata mama yangu baada ya kuona tukio na kumwelekeza akasema inawezekana mwanangu unajitabiria kuoa. Kwahiyo mama yangu amefurahi sana, mimi napenda kuwa na mahusiano na mtu ambaye ni mshikaji wangu,” aliongeza.
Kwa upande wa model, Erica aliyepiga picha na Linex alisema yeye na Linex ni wapenzi wa muda mrefu.
“Kufanya shooting na Linex nimejisikia poa kwa sababu ni msanii mkubwa. Mimi na Linex kabla ya hii kazi ni wapenzi na mpaka sasa ni wapenzi.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.