Olamide na Don Jazzy Wamaliza Bifu Lao Kimyakimya ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Olamide na Don Jazzy Wamaliza Bifu Lao Kimyakimya !

donDon Jazzy na Olamide wakipeana mikono.
HABARI ya ‘mujini’ mwaka huu kwa wapenda muziki nchini Nigeria na kwengineko duniani ni kumalizika kwa bifu la muda mrefu kati ya maprodyuza  wakubwa,  Olamide na Don Jazzy.  Baada ya wawili hao kutokea katika picha wakiwa wameshikana mikono, mashabiki wamebaki kujiuliza ni wapi walipolimalizia ugomvi wao wa muda mrefu?.
Katika picha hiyo kulikuwa na maandishi yaliyowaomba msamaha mashabiki wao kwa bifu lililokuwepo na kwamba wajibu wao ni kuongoza lakini walifanya makosa ya kufanyiana uhasama kwani na wao ni binadamu.
Itakumbukwa kwamba katika tambo zake, Olamide alimwambia Don Jazzy aendeshe shughuli zake kwenye eneo lake (kisiwani)  bila kumwingilia kikazi katika himaya yake (bara).  Hata hivyo, hivi sasa wamepatana na mashabiki wanajiuliza walikutana wapi ‘wakamalizana’, kisiwani au bara?

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.