Messi Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia​ ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Messi Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia​ !

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya soka ya Barcelona nchini Hispania, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ikiwa mara yake ya tano kushinda tuzo hiyo.
Messi ameshinda kwa kupata asilimia 41.33 ya kura zote na kumuacha kwa mbali mpinzani wake karibu, Christiano Ronaldo aliepata asilimia 27.76 na mchezaji mwenzake wa klabu ya Barcelona, Neymar.
Mwaka 2015 Messi amefunga magoli 52 kwa mechi 61 alizocheza na kusaidia magoli(assists) 27, akishinda magoli kwenye michuano yote sita ambayo timu yake imeshiriki na kushinda 
mitano.
Washindi 15 wa tuzo hio kwa miaka 15 ya mwisho ni Luis Figo(2000), Michael Owen(2001), Ronaldo(2002), Pavel Nedved(2003), Andriy Shevchenko(2004), Ronaldinho(2005), Fabio Cannavaro(2006), Kaka(2007), Cristiano Ronaldo(2008), Lionel Messi(2009), Lionel Messi(2010), Lionel Messi(2011), Lionel Messi(2012), Cristiano Ronaldo(2013), Cristiano Ronaldo(2014) na Lionel Messi(2015)
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.