Man City kuivaa Liverpool fainali ya Capital One Cup - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man City kuivaa Liverpool fainali ya Capital One Cup

Bet Sasa
Aguero akiifungia Man City bao la tatu katika mchezo wa Capital One Cup dhidi ya Everton.
Aguero akiifungia Man City bao la tatu katika mchezo wa Capital One Cup dhidi ya Everton.
Goli la kichwa la Sergio Aguero dhidi ya Everton kwenye dimba la Etihad limeipeleka Manchester City kwenye fainali ya michuano ya Capital One Cup.
Everton waliingia kwenye game hiyo wakiwa mbele kwa aggregate ya bao 2-1  lakini Ross Barkley aliongeza gape hilo kwa kupachika bao la mapema kwenye uwanja wa Etihad na kuipa City kazi nyingine ya ziada na kufanya Everton kuwa mbele kwa aggregate ya mabao 3-1 mbele ya Man City.
Fernandinho alisawazisha bao hilo na kuirejesha timu yake mchezoni baada ya shuti lake kumgonga beki wa Everton na kujaa kambani.
Bao alilofunga Kevin De Bruyne lilizua utata kwasababu Rahim Sterling alitoa pasi ya goli huku mpira ukiwa umeshavuka mstari wakutoka nje.
Bao alilofunga Kevin De Bruyne lilizua utata kutokana na pasi ya mpira aliyoipiga  Rahim Sterling  ilikuwa imeshavuka mstari wakutoka nje.
Kevin De Bruyne aliyeingia akitokea benchi alikunganisha krosi ya Raheem Sterling na kuiweka mbele Man City kwa bao 2-1 lakini aggregate ikisoma 3-3.
Aguero alipachika wavuni bao lililoipa ushindi City kutokana na pasi nzuri kutoka kwa De Bruyne.
Kiungo huyo wa Ubeligiji baadaye alitolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kuangua vibaya wakati anawania mpira na Ramiro Funes Mori.
Man City watacheza na Liverpool mchezo wa fainali ya kombe la Capital One February 28 mwaka huu kwenye uwanja wa Wembley.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.