Kumbe Wayne Rooney Alimbania RONALDO Kutwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Duniani "BALLON D’OR" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kumbe Wayne Rooney Alimbania RONALDO Kutwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Duniani "BALLON D’OR"

Bet Sasa
Tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or imefikia tamati jana na kushuhudia mchezaji Lionel Messi akiitwaa tuzo hiyo kwa mara ya tano na kuweka rekodi kuwa mchezaji pekee kuwahi kutwaa tuzo tano tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo.
Lakini moja ya kura zinazompitisha mshindi wa tuzo hii ni kura kutoka kwa makocha wa timu za taifa na manahodha wa timu za taifa na wadau wengine maalumu.
Wayne Rooney ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya England ameteka vyombo vya habari mara baada ya kugundulika kuwa alimpigia kura Lionel Messi na Thomas Muller mbele ya mchezaji mwenzake wa zamani Cristiano Ronaldo, kitu ambacho kimevuta hisia za wadau mbalimbali wa soka.
Lakini kipengele kingine kinachogombaniwa katika tuzo hizo za kila mwaka za FIFA, ni kutafutwa kwa kocha bora wa msimu, tuzo ambayo hivi sasa imetwaliwa na kocha Luis Enrique wa Barcelona mara baada ya kushinda vikombe vyote ilivyoshiriki timu yake ya Barcelona.
Mwezi uliopita ikiwa stori za kocha Jose Mourinho zikizagaa kujiunga na klabu ya Manchester United, nahodha huyo wa England na Manchester United aliwachagua Jose Mourinho, Pep Guadiola na kocha wa timu ya taifa ya Chile George Sampaoli, na kumuacha kocha Luiz Enrique ambaye aliisaidia Barcelona kutwaa makombe hayo yote.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.