Kidoa Na Samatta Wanaswa ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kidoa Na Samatta Wanaswa !

Video Queen Asha Salum ‘Kidoa’ akipozi na Samatta.
Baada ya hivi karibuni Video Queen Asha Salum ‘Kidoa’ kuibuka na kueleza kuwa, yuko tayari kufanya lolote ili awe na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ kimapenzi, mdada huyo amenaswa tena juzikati akiwa na mwanasoka Mbwana Samatta hotelini.

Saa 5 usiku
Mishale ya saa 5.30 usiku, chanzo chetu kilichokuwa maeneo ya Hoteli ya Girrafe iliyopo Mbezi jijini Dar Jumapili iliyopita, kilitutonya kuwa kilikuwa kikiwaona wawili hao wakizama hotelini hapo bila kujulikana kilichowapeleka.

“Ee bwana nipo hapa Girrafe Hoteli, ila naomba nisijulikane kama nimewapa taarifa, ni hivi muda mrefu nimemuona Mbwana Samatta na yule mrembo mwenye makalio makubwa sijui anaitwa Kidoo….
Ijumaa: Siyo Kidoo, anaitwa Kidoa.
Chanzo: Ndiyo, huyo huyo.
Ijumaa: Endelea…
Chanzo: Ndiyo nawaona wako katika eneo la restaurant (hotelini), kama ni habari kwenu njooni mtawakuta.
Ijumaa: Wako katika mazingira gani?
Chanzo: Naomba kama mnahitaji habari mje tu usiniulize maswali mengi maana nitashitukiwa, wahini kabla hawajaondoka.
Ijumaa: Oke, poa tunakuja
Baada ya kupata taarifa hiyo, waandishi wetu walichukua usafiri wao wa pikipiki ziendazo kasi na kuanza safari ya kuelekea Mbezi.
Wakati paparazi wetu wakielekea eneo la tukio, simu ya mmoja wao ikaita, alikuwa yule sosi wa habari hiyo.


Kidoa na Samata wakiondoka hotelini.

Chanzo: Mbona mnachelewa? Naona wanainuka kama wanataka kuondoka hivi. Wanaonekana kuwa wenye furaha sana. Naona wanapiga picha, Kidoa anamsogelea. Kwa kifupi wanafanya yao.
Ijumaa: Hebu wafotoe picha hata kwa kamera ya simu yako.
Chanzo: Sawa, ngoja nijaribu kufanya hivyo.

Saa 6 usiku
Mishale ya saa sita usiku, paparazi wetu wakawa wamefika hotelini hapo na kukuta wawili hao wakiingia kwenye gari aina ya Toyota Mark X nyeusi kisha kuondoka zao kuelekea kusikojulikana.

Wenyewe wanasemaje?
Jitihada za kuwasaka mastaa hao zilifanyika ambapo Samatta hakuweza kupatikana kupitia simu yake ya mkononi lakini Kidoa alipopatikana alikiri kufika hotelini hapo kwa mazungumzo ya kawaida na mwanasoka huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa.
“Ni kweli tulienda pale, hakukuwa na chochote zaidi ya mazungumzo ya kawaida tu na tuliishia restaurant tu, hakuna lolote. Yule najuana naye muda mrefu mbona, msidhani nampapatikia kwa sababu ya tuzo aliyopata,” alisema Kidoa.

Hivi karibuni, Samatta aliitoa kimasomaso Tanzania baada ya kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, iliyofanyika nchini Nigeria na kuweka historia ya kuwa Mbongo wa kwanza kupata heshima.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.