Jokate, Kiba Kumwagana Kumbe Chanzo Ni Mimba. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jokate, Kiba Kumwagana Kumbe Chanzo Ni Mimba.

Wakati mastaa wenzake Bongo, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja wakifurahia kunasa ujauzito, taarifa ambazo zimevuja zinadai kwamba, chanzo cha Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ kumwagana na Mwanamuziki Ali Saleh Kiba ni kufuatia kuchoropoka kwa mimba ya mrembo huyo hivyo kumsononesha moyo wake, Ijumaa limenyetishiwa siri nzito.
Habari kutoka ‘redio mbao’ za mjini zilidai kwamba, wiki mbili zilizopita, Jokate na Kiba waliingia kwenye gogoro zito mara tu baada ya kuripotiwa kuchoropoka kwa ujauzito huo ikisemekana kuwa hali hiyo ilimpata kufuatia kufanya mazoezi makali ya kudensi akijiandaa na shoo.
“Unajua Kiba aliposikia mimba ya Jokate ambayo aliamini ni yake imechoropoka, alihisi anafanyiwa figisufigisu na kwamba huenda Jojo hakuwa amejiandaa kuitwa mama,” kilidai chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina na kuongeza:
“Ndiyo chanzo cha ugomvi wa Jokate na Kiba licha ya zile sababu nyingine za tofauti ya dini, wazazi wa Jokate kutomtaka Kiba. Bado vikao vya kuwasuluhisha vinaendelea lakini jamaa (Kiba) anaonekana kutia ngumu.”
Hata hivyo, habari mpya zilizolifikia gazeti hili zilidai kuwa kumwagana kwa Jokate na Kiba kulipokelewa kwa kicheko na ndugu wa mrembo huyo ambao tangu awali walionekana kutounga mkono penzi la wawili hao.
Gazeti hili lilipomtafuta Kiba ili kufafanua ishu hiyo, kama kawaida simu yake iliita bila kupokelewa lakini kwa upande wake Jokate alikuwa na haya ya kusema: “Jamani naombeni mniache, sitaki kabisa kuongelea hayo mambo ya Ali Kiba.”
Hata hivyo, mwanahabari wetu alipotaka kusikia japo neno lake juu ya kuachana na Kiba na kwamba chanzo ni kuchoropoka kwa ujauzito huo, alisisitza kwamba aachwe.
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.