GigyMoney Adai Kuporwa AliKiba Wake ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

GigyMoney Adai Kuporwa AliKiba Wake !

Giggy-Money
MUUZA nyago machachari Bongo Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameonekana kushobokea penzi la Mwanamuziki Ally Salehe Kiba kwa kudai kuwa eti alikuwa wake ila Jokate Mwegelo akampora.
Akipiga stori na paparazi wetu huku akionesha picha mbalimbali alizopiga naye, Gigy alisema kuwa alishangazwa sana na taarifa kuwa, Jokate yuko na Kiba wakati yeye ndiye aliyekuwa amejiweka kwake.
“Watu hawajui ila Kiba alikuwa wangu, Jokate kanipora,” alisema Gigy huku akionekana kutumia picha alizopiga na staa huyo kama ushahidi wa uhusiano wao.
Jitihada za kumpata Ali Kiba hazikuzaa matunda ila Jokate alipopatikana alijibu kwa kifupi: “Hata hatumjui huyo Gigy na wala sipendi kuandikwa naye.”

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.