Gigy Money na Tekno Wa "DURO" Mambo Wazi Wazi ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gigy Money na Tekno Wa "DURO" Mambo Wazi Wazi !

Bet Sasa
IMG-20160101-WA0022
Mrembo anayeuza sura kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameibua gumzo baada ya ukweli kuanikwa kwamba alilala kwenye Hoteli ya Serena iliyopo Posta jijini Dar akijiachia na msanii kutoka Nigeria, Tekno Miles.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, usiku wa kuamkia Ijumaa, mrembo huyo alionekana akijiachia na jamaa huyo ambaye alitua Bongo kwa ajili ya kutumbuiza kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kwamba, katika kudhihirisha hilo, Gigy alitupia picha kadhaa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na Tekno hivyo kupewa makavu laivu na mashabiki wakionesha kwamba kitendo hicho ni kujidhalilisha kwa kumshobokea staa huyo wa Ngoma ya Duro.
IMG-20160101-WA0024Kufuatia ishu hiyo, gazeti hili lilimsaka Gigy ili afunguke juu ya tukio hilo ambapo alikiri kukutana na kulala na jamaa huyo hotelini hapo.
“Wanaoponda waache waongee tu, mimi sirembi hata kidogo pale ninapotaka jambo langu litimie, ingekuwa nimegharamia kulipia hoteli sawa, lakini sijahusika hata kidogo na hilo, wamelipa wenyewe,” alisema.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.