Faiza aoga matusi kwa kupost video inayodaiwa kumdhalilisha mwanae pamoja na Mh. Sugu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Faiza aoga matusi kwa kupost video inayodaiwa kumdhalilisha mwanae pamoja na Mh. Sugu

Faiza Ally is at it again! Muigizaji huyo controversial ameyaoga matusi kutoka kwa watu mbalimbali baada ya kupost kwenye Instagram video ambayo wengi wanahisi sio sawa.
Mama huyo wa mtoto mmoja amepost video inayomuonesha mwanae Sasha akilia na kumtaka baba yake ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini amtumie fedha.
“Baba anitumie hela nikasuke,” anasikika Sasha akisema kwenye video hiyo na mama yake ambaye haonekani akimuuliza, “baba yako anaitwa nani?” Sasha anajibu, “Joseph Mbilinyi” na kasha kuendelea kulia kwa uchungu.
“Anayemjua baba wa huyu mtoto amwambie analilia kusuka….. Anaomba baba yake amtumie hela kwa kuwa sina mawasiliano naye hopeful mtamfikishia ujumbe….. Na mimi ndio hivyo tena leo sina chapaa,”ameandika Faiza kwenye video hiyo.
Hata hivyo, wengi hawajapendezwa na kitendo hicho walichokitafsiri kama cha udhalilishaji.
“Ndo shida ya kuzaa na makahaba, yaan ni upuuzi mtupu. Huyo baba wa mtoto alikupea mimba humu insta? Hizo ndo haki za mtoto mnavyomdhalilisha humu kwenye mitandao? mheshimiwa alimchukua mwanae kwa madai malezi anayoyapata kwa mama hayastahili kwa mtoto, lkn wabunge wanawake wakapiga kelele kupaza sauti kuwa huyu mwanamke ameonewa kwa kunyang’anywa mtoto.sasa hebu oneni huyo aliyedai anaonewa.huyo mtoto mmemfedhehesha sn.kama mama huna hela yakumpa mtoto akasuke si basi, bado unapost uko na mwanaume mwingine, hv nani akuelewe?? Namuhurumia sana huyo mtoto,” ameandika mmoja.
Mwingine ameandika: Hapana Faiza leo umekosea! Kwel japo ni mtoto ila unamkosea, hapana!! Tunakupenda ila this is too much.”

Wapo wachache waliomsupport pia kama huyu: Mi naona mnachokisema ni tofauti Na alichokilenga Faiza,kwanza hii post was for fun,make kama anaweza kumlipia ada atashindwa hela ya nywele?Ila alitaka kushare Na kina mama ambao Mara nyingi watoto wetu huwa akingangania kitu mpaka Analia bila kujua kama mama ana hela au hapana.”

Hata hivyo baada ya matusi kuwa mengi, Faiza aliamua kurudi tena na post ndefu:
NYINYI MNAOSEMA KAMA NIMESHINDWA KUMLEA MTOTO NIMUACHIA BABA YAKE- NAWAONA WA**BAVU TU KAMA WA***BAVU WENGINE WOTE….. KUTAKA KUISHI NA MWANANGU SIO SABABU YA BABA KUTOKUJUA MTOTO ANA KAA WAPI! ANAKULA NINI- ADA ANAPATA WAPI NA SHULE ANA SOMA IPI… NDIO NINA HAKI YA KUKAA NA MWANANGU LKN SIO KWAMBA KWA SABABU NAISHI NAE NDIO SABABU YA KUTOMKUTUNZA MWANAE….
NA P**BAVU ZENU WALE WANAO SEMA NA MZALILISHA SASA MNTAKA NIMPEJE UJUMBE IKIWA SINA MAWASILIANO NAE ? KAMA SIO KUTUMIA MITANDAO ….. ? NAO MNAOSEMA NIMESHINDWA MNAJUA NALIPA KODI KIASI GANI? ADA SH NGAPI ? MATUMIZI NA MNAJUA NAPATAJE MANINA ZENU? AU MNAZANI KUWA SINGLE MAMA MCHEZO – P**AVU ZENU NYOTE MNAO SHANGAA MIMI KUONYESHA HISIA ZANGU…..
KUNA NYAKATI ZINGINE UNASHINDWA KUJIZUIA UKIWA KAMA MZAZI UNAPO KOSA MSAADA WOWOTE KWA MZAZI MWENZIO SPECIAL AKIWA NA UWEZO WA KUTOA…. NA SI KWAMBA NIMESHINDWA ILA NIMEKASIRIKA NA KUSIKITIKA SANA PALE MWANANGU ANAPO HITAJI NA NAKUA SINA KWA WAKATI HUO NA NIKITIZAMA BABA YAKE ANAO UWEZO LKN ANA NIKOMOA KWA AJILIA YA KUMUACHA – HII HAINGILIANI KABISA NA KUTO KUMJALI MWANANO- NA ZAIDI AKIWA AMESIMAMA BUNGENI KUTETEA WANANCHI IKIWA VIZAZI VYAKE VINA HANGAIKA IKIWA KAKA YAKE SASHA AMBAE AMEMTOA MJINI BAADA KUJULIKANA NA KUMPELEKA MTWARA AMEKUA MLEVI HUKO WKT BORA ANGEMUACHA HAPA GARAGE ALIKUA ANA JIPATIA RIZIKI YAKE …… WANAO WOTE WAWILI HAWAJALI …..
KAMA MZAZI INAUMA …… NYIO MSIO JUA UCHUNGU WA MTOTO WALA UGUMU WA KUWA SINGO MAZA FUNGENI MIDOMO YENU VISEBENGO WAKUBWA SUBIRI YENU !!!!!!!!!!! NA BAADA YA YOTE KUNIPELEKA MAHAKANI NATOA HELA ZANGU NA KESI INAZUNGUSHWA….. KILA NINAPO FIKA MAHAKAMANI LZM NILIPE NA ADA YA MWANASHERIA m.2 …… KAMA SIO KUKOSA UBINAADAMU NI NINI ????? – SIKILIZENI SINA ASILI YA KITUMWA NIKO KATIKA TAIFA HURU NA NITASEMA NA KUFANYA KILE NINACHO AMINI….. NA NINA AMINI KIONGOZI BORA ANA ANZIA NYUMBANI……….. LKN MWISHO WA SIKU YOTE MAISHA NITASIMAMA TU NA NITAWEZA LKN WKT MWINGINE BINAADAMU LZM TUSEME YALIYO MOYONI ILI TUENDELEE NA YAJAYO…… NARUDIA TENA KWA YOYOTE ANAE SHANGAA HILI NI M**BAVU NA AMETOKA KWENYE FAMILIA ZA KINAFKI ZINAZO FUNIKAGA VITU AMBAVYO HAVI STAHILI KUFUNIKWA!!!!!!!!!!!!!

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.