Fahamu kuhusu Mzee Yusuf kutaka kuimba Hip Hop kabla hajaanza kufanya Taarab. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Fahamu kuhusu Mzee Yusuf kutaka kuimba Hip Hop kabla hajaanza kufanya Taarab.

14 - 17
Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Allan Mapigo amedai wakati wanakutana na Mzee Yusuf kwa mara ya kwanza ili amrekodie wimbo wake, msanii huyo wa Taarab alikuwa anataka kufanya muziki wa Hip Hop.
Mapigo ameiambia Bongo5 kuwa yeye ni miongoni mwa watarashaji wa zamani waliosupport muziki wa Tanzania hadi kufika hapa ulipo.
“Nimesaidia wengi sana kwenye huu muziki toka zamani, akina AT, Berry Black, akina Bella, Ray C , Mzee Yusuf,” alisema.
“Nakumbuka kwa mara ya kwanza Mzee Yusuf anakuja kwenye studio yangu alikuwa anataka arekodi wimbo wa Hip Hop mimi nikamwambia wewe unafaa kwenye mduara ndio akaanza kurekodi nyimbo za mduara na mimi ndiye niliyemfanyia album yake ya kwanza. Kwahiyo mimi ni miongoni mwa watayarishaji wa zamani ambao tuliweza kuwashape wasanii wengi mpaka leo hii unaona wanafanya fanya vizuri,” aliongeza.
Mtayarishaji huyo amesema kuwa sasa anajiweka sawa ili aje kivingine kwani anaamini kuwa bado ana nafasi kubwa katika muziki huu.

-Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.