Diamond Platnumz ana mtoto mwingine Mwanza ambaye ni mkubwa wake Tiffah ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Platnumz ana mtoto mwingine Mwanza ambaye ni mkubwa wake Tiffah !

post-feature-image
Tiffah Dangote ana ndugu yake, aliyezaliwa na msichana aliyekutana kimapenzi na baba yake (one night stand), Diamond Platnumz enzi anaanza kuupata ustaa.

Taarifa hizo zilitolewa hivi karibuni na Diamond mwenyewe wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Papaso cha TBC FM. Anasema tukio hilo lilitokea mwaka 2010, Mwanza alikoenda kufanya show.

Huyo mwanamke story ilivyokuwa alikuwa ametoka kwenye chumba cha brother Dully akaja kwangu mimi nikafanya yangu, mimi nikarudi huku mtoto akawa ananimbia ‘ebwana mimi nina mimba,” alisimulia Diamond.

Basi ilivyokuwa mtoto ‘bana eeh mimi nina mimba’ na mimi nikawa nachezesha nini nikawa namhudumia, huku na huku bahati mbaya nikaanza na demu fulani hivi kwahiyo demu mwenyewe akanimind, nikawa nampigia simu hapokei nikaenda Mwanza kumsakanya huku na huhu nasikia kwao wakanimind nikaonekana kama mimi nazingua,”alisema.

Siku moja nikaenda nikambanabana ‘nikamwambia wewe una mtoto’ akanikatalia kwasababu aliniambia ile mimba niliitoa nini, kumbe ni muongo. Nikaja nikamchunguza kumbe alikuwa amezaa na mtoto namuambia ‘nataka basi nimuone mwanangu’ alinikatalia sana lakini baadaye akaja kuniambia ni kweli ni mwanao umefanana naye na nini. Nikamwambia namuomba nimuone kwenye picha huku na huku hakuweza kuwa nayo.

Ikabidi asubuhi alipotoka hotelini akaenda kuniletea picha za mwanangu nione. Sasa wakati anakuja akaja amechelewa kwasababu mimi ndege yangu ilikuwa imeshakaribia ikabidi mimi nikarudi nikaacha vitu vyake pale reception, kurudi nampigia simu nitumie kwenye email sasa suala likaishia hivyo, yaani kila nikimpigia hapokei.

Kwa maelezo yake inaonesha kuwa Diamond hajawahi kumuona mtoto wake huyo tangu azaliwe.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.