Diamond aajiri msomi amkatikie mauno ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond aajiri msomi amkatikie mauno !

Hii ni zaidi ya kufuru! Mwanamuziki aliyejipatia umaarufu mkubwa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ukipenda muite Simba ameweka historia kwenye ulimwengu wa muziki wa Bongo Fleva kwa kumuajiri binti msomi aitwaye Zaituni Musa Bakari ili amkatie mauno kwenye shoo zake.
IMG_7464
Binti msomi aitwaye Zaituni Musa Bakari akimkatikia mauno Diamond Platinumz.
Ni dansa tegemezi
Zaituni, binti aliyejaaliwa kuwa na figa bomba, alianza kufanya kazi na Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB) muda mrefu lakini hivi karibuni wakati akiendelea kunengua, alijiunga na Chuo cha Biashara cha CBE jijini Dar akichukua Stashada ya Manunuzi na Ugavi (Diploma in Procurement and Supply).
Inadaiwa wakati akisoma chuoni hapo ni wachache waliokuwa wakijua kuwa anasoma hivyo kumfanya afanye mambo hayo mawili kwa wakati mmoja kwa makini.
Hata hivyo, mwaka 2015 baada ya kuhitimu masomo yake ndipo siri ikavuja kuwa, mdada huyo ni msomi na ndipo alipoanza kuwa gumzo kila kona ya Jiji la Dar es Salaam.
Analipwa mshahara mkubwa
Chanzo kilicho ndani ya WCB kilidai kuwa, mshahara anaovuta mdada huyo ni mkubwa kutofautisha na wengine ndiyo maana licha ya kuhitimu, bado anaendelea kunengua.
“Unajua yule binti anajua sana kukata mauno na ni mtu muhimu sana kwenye kundi la madansa. Ukifuatilia kwenye shoo nyingi ndiye ambaye mara nyingi hucheza na Diamond huku akimkatikia, mshahara wake ni mkubwa sana,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta mdada huyo na alipopatikana mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Ijumaa: Ni lini ulianza kufanya kazi hii?
Zaituni: Nilianza kudansi nilipomaliza kidato cha nne na baadaye nikaja kula shavu kwenye kundi hili la madansa wa Diamond.
IMG_0151
Zaituni Musa Bakariakiwa katika pozi.
Ijumaa: Ilikuwaje ukajiingiza kwenye kazi hii ambayo baadhi huidharau?
Zaituni: Ni kitu ambacho kilikuwa kwenye damu yangu, napenda kudansi na najua kudansi hivyo nilipopata nafasi ya kuja kufanya kazi na WCB, sikusita na wala sikusikiliza maneno ya watu.
Ijumaa: Shepu yako inaonekana umejaaliwa, unawezaje kumudu kufanya mavituz jukwaani?
Zaituni: Kikubwa ni mazoezi, nafanya mazoezi sana ndiyo maana naumudu mwili wangu.
Ijumaa: Wewe ni msomi, umesomea mambo ya Manunuzi na Ugavi, kwa nini usiende kufanya kazi hiyo?
Zaituni: Hayo mambo yatakuja baadaye lakini kwa sasa nafanya kazi hii na nina mpango wa kwenda kuchukua shahada katika fani hiyo.
Ijumaa: Inasemekana wewe ndiye unayelipwa mshahara mkubwa sana kwenye wale madansa pale WCB, kuna ukweli wowote?
Zaituni: Kwa kweli sijui maana si unajua mshahara ni siri ya mtu, huenda ikawa hivyo lakini sina jibu la moja kwa moja.
Ijumaa: Kwani unalipwa kiasi gani?
Zaituni: Hiyo sasa ni siri yangu kaka.
Baada ya kuzungumza na dansa huyo, Ijumaa lilimtafuta Diamond kumzungumzia dansa wake huyo msomi ambapo alisema anajisikia poa kufanya naye kazi na anaamini ana mapenzi na kazi hiyo ndiyo maana amekubali kuwa WCB.
Kuhusu madai kuwa analipwa msharaha mkubwa, Diamond alisema hiyo ni siri kati ya muajiri na muajiriwa.

Chanzo: GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.