Davido Atoka Hospitalini Nchini Gambia ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Davido Atoka Hospitalini Nchini Gambia !

davido-beards
MWANAMUZIKI staa wa Nigeria, Davido, aliyekuwa nchini Gambia hivi karibuni, alishindwa kuhudhuria tamasha la tuzo za wanamuziki la Headies Award kutokana na uchovu ambapo ilibidi alazwe hospitalini.
Akijibu swali kwa nini hakuhudhuria tamasha hilo, Davido alisema hakuona sababu yoyote ya kufanya hivyo  kwani hata tuzo tatu alizoshindwa mwaka 2014 hadi leo hajapewa.
“Nilikuwa Gambia, kaka, lakini hata tuzo tatu nilizoshinda mwaka jana, hazijatua mikononi mwangu,” alisema Davido akimjibu mwandishi mmoja wa habari, akiongeza kwamba hivi karibuni ataingia studio kufanya ‘remix’ ya wimbo wa ‘Osinachi’ wa Humble Smith.
“Mungu ndiyo nguvu yangu.  Baada ya kuondoka hospitalini, nitaufanyia remix wimbo wa ‘Osinanchi’,” alisema.
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.