Chris Brown Aingia Kwenye Msala Mpya ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chris Brown Aingia Kwenye Msala Mpya !

Chris Brown ni mtuhumiwa wa kumpiga na kumjeruhi mtu pamoja na wizi uliotokea Jumamosi iliyopita kwenye kiota cha Palms Casino Resort, jijini Las Vegas.
Chris-Brown-PNG
Polisi wanadaiwa kuitwa hapo asubuhi na walimkuta mwanamke aliyekuwa na majereha mwilini mwake kufuatia kupigwa.
Kwa mujibu wa The Hollywood Reporter, mwanamke huyo anadai kupigwa na Chris Brown baada ya kuchukua simu yake kupiga naye picha. Anadai kuwa muimbaji huyo alichukua simu yake.
Mwakilishi wa Brown alidai kuwa tuhuma hizo si za kweli.
Alisema kuwa mwanamke huyo aliondolewa kwenye party ya faragha kutokana kuonesha tabia chafu na hivyo aliamua kusema uongo kulipiza kisasi.

“Her claim that she had her phone in her possession inside the after party and was able to take a photo causing an altercation with Chris Brown is a complete fabrication,”
yalisema maelezo.

“This seems like a clear case of retaliation for her bruised ego.”
Upelelezi zaidi unaendelea.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.