Arsenal Wanunua Kiungo wa FC Basel - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Arsenal Wanunua Kiungo wa FC Basel

Elneny
Elneny anaweza kuchezea Arsenal dhidi ya Stoke Jumapili
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel Mohamed Elneny.

Mchezaji huyo anaweza kuwachezea dhidi ya Stoke Jumapili.

Elneny, 23, anaripotiwa kuwagharimu Gunners £5m na anahitimu kuwachezea katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Akizungumza baada ya Arsenal kutoka sare ya 3-3 na Liverpool uwanjani Anfield, Wenger alisema: "Amejiunga nasi na tutamchunguza kuona iwapo anatosha kucheza Jumapili.”
Elneny alichezea Basel mechi ambayo walilaza Chelsea msimu wa 2013-14. Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.