Alikiba anaamini kutoa nyimbo nyingi ni kutojiamini. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba anaamini kutoa nyimbo nyingi ni kutojiamini.

alikiba1
Hitmaker wa Mwana, Alikiba amedai yeye anaamini kutoa nyimbo mara kwa mara ni kutokujiani na ufujaji wa kipaji. 
Muimbaji huyo ambaye amekuwa akishinikizwa na mashabiki wake kuachia wimbo mpya ikiwa ni miezi kadhaa toka aachie video ya wimbo ‘Cheketua’, alikiambia kipindi cha The Sporah Show cha Clouds TV kuwa yeye akitoa kazi yake moja ina uwezo wa kukaa sokoni kwa muda mrefu.
“Fans don’t worry about me, kitu ambacho nafanya ‘New Kiba New Year’ ni kutaka kwenda sawa na nyie. Lakini nilikua nataka mnielewe kutoa nyimbo kila dakika ni umalizaji wa talent yako au kutokujiamini au talent yako fupi au una jaribu. Mimi najiamini kwa kitu ambacho natoa na ni muda gani natakiwa kurudi tena,” alisema.
Aidha, Alikiba aliwataka watu kuacha kumfananisha na wasanii wengine kwakuwa yeye anafanya vitu tofauti na wengine.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.