Ujenzi Wa Mjengo Wa Jux Wakwama , Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ujenzi Wa Mjengo Wa Jux Wakwama , Ipo Hapa

Mkali wa ‘One More Night’ Jux ameeleza sababu ya kukwama kuendelea kwa ujenzi wa mjengo wake wa kifahari ambao miezi kadhaa aliuonesha kwenye mitandao ya kijamii.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa kwa sasa amesimama kidogo kuendeleza mjengo wake na kuwekeza pesa katika kufanya muziki ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya video zenye ubora.
Maponda
“Unajua kwa sasa kidogo nimesimama kuendeleza nyumba hivyo, ipo siku watu watakuja kuona mjengo ukiwa umekamilika maana maisha yetu sisi wasanii hayawezi kufichika. Nimesimama sababu pesa ninazopata nimezielekeza katika kufanya muziki na video kali,” alisema Jux.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alieleza jinsi anavyoweza kufanya video kali zinazomgharimu pesa nyingi wakati haonekani akifanya show nyingi kama wasanii wengine.
“Ni kweli hata Jumatatu (jana) nitaondoka na kurudi shule nchini China, lakini kwa sasa ninachofanya ni kuwekeza katika muziki huku nikiamini baadaye hiki ninachofanya sasa kitanilipa. Hivyo najenga ukaribu na mashabiki wangu na Mungu akijalia nikamaliza masomo yangu nchini China nitaanza kufanya show za uhakika. Unakuta hata sasa hivi natafutwa sana ili nifanye show lakini bahati mbaya huwa nakuwa nje ya nchi na kuzikosa show hizo,” alifafanua.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.