Ufisadi Mwingine Wa Bilioni 48 Waibuliwa Bandarini, 7 Watiwa Mbaroni, 8 Wanasakwa na Jeshi la Polisi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ufisadi Mwingine Wa Bilioni 48 Waibuliwa Bandarini, 7 Watiwa Mbaroni, 8 Wanasakwa na Jeshi la Polisi

Serikali imepoteza jumla ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.

  
Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.
  
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawaamesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.
  
Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh 47.4 bilioni wakati magari gari 2019 zenye thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.


-udakuspecial 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.