SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA MFUMO MPYA WA KISASA WA USIMAMIZI WA MIZIGO KWENYE VIWANJA VYAKE VYA NDEGE. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA MFUMO MPYA WA KISASA WA USIMAMIZI WA MIZIGO KWENYE VIWANJA VYAKE VYA NDEGE.

Bet Sasa
Shirika la ndege la Etihad ambalo ndio shirika rasmi la nchi ya Falme za kiarabu, leo hii limetangaza makubaliano na kampuni ya Luggage Logistics kuboresha mfumo mzima wa usimamizi wa mizigo katika viwanja vake vya ndege dunia nzima.
Kupitia mfumo wa kisasa wa Baggage Management System (BMS) unaosimamiwa na kampuni ya Luggage Logistics, shirika la ndege la Etihad litaweza kuboresha usimamizi ikiwemo kusafirisha mizigo ya wasafiri kwa wakati. Mfumo huo pia utawezesha kufuatilia kwa urahisi mizigo iliypotea njiani dunia nzima.
Mfumo wa BMS utahusisha ratiba za ndege, taarifa za wasafiri pamoja na mifumo ya udihibiti safari zote ka pamoja. Hii itasaidia kuongeza kasi taratibu za kutambua mizigo ya abiria  na kisha kuhamisha mizigo toka kwenye ndege hadi uwanja wa ndege na hatimaye kwenda kwenye ndege ya kuunganisha safari husika, ikisaidia safari kutochelewa.
Mfumo huu umeunganishwa katika kituo kimoja cha udhibiti ambapo taarifa zote za mizigo kutoka vyanzo mbalimbali hutunzwa. Taarifa hizi zinaweza kusambazwa haraka na uwepesi baina ya vitengo husika dunia nzima
Geert W. Boven, Makamu rais wa Huduma za viwanja vya ndege kutoka Etihad, alisema: “Ushirikiano na kampuni ya Luggage Logistics kutaongeza ufanisi zaidi katika kutambua, kusimamia na kusafirisha mizigo ya abiria duniani kote kwenye viwanja vyetu tukianzia na hapa Abu Dhabi. Mfumo mpya huu utasaidia kuboresha huduma kwa abiria kwa kupunguza upotevu wa mizigo, kupunguza idadi ya safari zinazochelewa juu ya kupotea kwa mizigo pamoja na kuongeza ufanisi wa huduma zetu za uwanja wa ndege”

Adam Dalby, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Luggage Logistics, alisema “Tunayofuraha kushirikiana na shirika la ndege la Etihad, shirika ambalo tupo pamoja katika kutambua umuhimu wa uvumbuzi na huduma bora. Kupitia mfumo huu wa kisasa wa BMS, taarifa za papo hapo hupatikana na hutumika kuhakikisha mizigo ya abiria inasimamiwa kwa ufanisi zaidi safari nzima”
Shirika la ndege la Etihad lilichagua mfumo wa BMS kwani unakidhi mahitaji na vigezo vyote vya usimamizi mizigo, ikiwemo ICAO Annex 17 pamoja na maazimio ya IATA, mfumo huu unaweza kuunganishwa na mitambo ya shirika hili la ndege bila ugumu wowote pia. Suluhisho hili limewiana na uendeshaji na mahitaji ya miundombinu ya Shirika la ndege nay ale ya kituo cha Abu Dhabi
- Mwisho -
 Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na  airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali 
tembelea :www.etihad.com

Kuhusu Luggage Logistics na Load & Track
Kmapuni ya Luggage Logistics ilianzishwa mwaka 2007, huku makao makuu yake yakipatikana Surrey Research Park in Guildford, Uingereza.  Luggage Logistics ni wataalamu wa kutoa huduma na ufumbuzi wa masuala ya anga ili kupata mifumo ya bei nafuu yenye kuongeza ufanisi katika sekta ya anga.  Wakitumia taarifa kutoka vyanzo mbali mbali, Load&Track wanatoa mfumo wa kisasa unaosimamia masuala ya mizigo kwa wateja wetu wote.

Kwa maelezo zaidi. :

Luggage Logistics
Asif Khan, Mawasiliano ya Kampuni
Barua pepe:  AsifK@etihad.ae
Adam Dalby, Mkurugenzi mtendaji

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.