Ommy Dimpoz "Niko Tayari Kuoa Hata Sasa, Kama Nikipata" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ommy Dimpoz "Niko Tayari Kuoa Hata Sasa, Kama Nikipata"

Staa wa Bongo Fleva,Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amesema kuwa yuko tayari kuoa hata sasa hivi kama nikipata mtu sahihi katika maisha yake.

Ommy ameyazungumza hayo wakati akiitambulisha video ya ngoma yake mpya iitwayo ‘Achia Bodi’ kwenye kipindi cha Clouds360  cha Clouds Tv wakati alipoulizwa na mtangazaji kipindi hicho Hudson Kamoga kuwa anatarajia kuoa lini.

Niko tayari kuoa hata sasa hivi kama nikipata mtu sahihi katika maisha yangu” Ommy Dimpoz.

Miezi ya hivi karibuni msanii huyo alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na msichana ambapo picha hizo zilizua maswali kwa mashabiki wake na kuuuliza huenda alikuwa ndiye shemeji yao,lakini hawakupata jibu.

Cloudsfm.com

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.