Mrembo Huyu Amchokonoa Jokate Kwa Kiba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mrembo Huyu Amchokonoa Jokate Kwa Kiba

ALI KIBA543
Habari ikufikie kuwa staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amewaka baada ya kutumiwa picha zinazomuonesha mwandani wake, Ali Saleh Kiba akiwa na mrembo aliyekuwa ‘akijibebisha’ kwa jamaa huyo akidai kwamba huko ni kumchokonoa ili watu waone atasema nini.
Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Jokate zilidai kwamba, alipoziona picha hizo za kimahaba za Kiba na mrembo huyo alipata mshtuko kiasi cha kutaka maelezo kutoka kwa staa huyo wa Ngoma ya Mwana.
jokate12
Hata hivyo, ilidaiwa kwamba katika utetezi wake, Kiba alimwambia Jokate kuwa mrembo huyo ataonekana kwenye video yake mpya aliyokuwa akishuti nje ya nje.
“Unajua Jokate ni mwelewa ‘so’ alipoambiwa hivyo alitulia lakini kabla ya utetezi huo hali ilikuwa mbaya maana alijua anaibiwa mali zake,” kilieleza chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Jokate ili kusikia upande wake ambapo alikiri kuziona picha hizo huku akishangaa ishu hiyo imelifikiaje gazeti hili.
“Ndiyo nimeziona kwani ninyi mmeipata wapi hiyo ishu? Any way mimi na Kiba tupo freshi,” alisema Jokate kwa kifupi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.