Jina La Kichanga wa Kim Kardashian na Kanye West Lashangaza Wengi, Hili Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jina La Kichanga wa Kim Kardashian na Kanye West Lashangaza Wengi, Hili Hapa

2-Good_guests_Also_at_the_event_were_Kim_Kardashian_and_Kanye_West-m-27_1441941286736.jpgKim Kardashian na mumewe Kanye West.kimNorth-West-curly-hairKanye West na Mwanaye, North Westrs_600x600-150303083544-600-north-west-yezzus.ls.3315_copyNorth West
MWANAMITINDO na mtangazaji wa Marekani, Kim Kardashian na mumewe ambaye ni mwanamuziki, Kanye West wamempa jina mtoto wao wa kiume aliyezaliwa hivi karibuni.
Wawili hao ambapo West hujulikana pia kwa jina la Yeezus na ambaye aliwahi kutoa wimbo uitwao ‘I Am God’ (Mimi ni Mungu), wamempa mwanao jina la ‘Saint West’ (Mtakatifu). Wanandoa hao tayari wana mtoto mwingine wa kike mwenye umri wa miaka miwili aitwaye North West.
Katika ukurasa wake wa mtandao, ambapo kichwa cha habari kilikuwa ‘Kwa Mashabiki Wetu’, Kardashian aliandika kwa kifupi tu  kwamba:  ‘Saint West, 12.05.15, 8 pounds 1 ounce’ akiwajulisha jina la mwanaye, tarehe aliyozaliwa na uzito wake.
Habari hizo zilizua utani kutoka kwa mashabiki wao ambapo wengine walituma picha zinazomwonyesha Maria na Joseph wakiwa wamepiga magoti kumtazama mtoto Yesu lakini sura zao zikiwa zimebandikwa na picha za Kardashian na Kanye West.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.