Hussein Machozi Atangaza Kuacha Muziki ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hussein Machozi Atangaza Kuacha Muziki !

Hussein Machozi ametangaza uamuzi wake wa kuacha kufanya muziki kutokana na kuona kwamba hakuna faida yoyote anayoipata kupitia muziki kwa muda mrefu .
hussein
Machozi ambaye jina lake halisi ni Hussein Rashid ni msanii wa Bongo fleva wa muda mrefu ambaye amewahi kutengeneza hits kadhaa ikiwemo ‘Kwaajili Yako, ‘Utaipenda’, Full Shangwe, na zingine.
Hussein ametangaza uamuzi huo kupitia Planet Bongo ya East Africa radio.
“Kubwa ambalo nataka niwasimulie Watanzania ambalo ninalo leo hii kwamba very soon ntaachia ngoma yangu mpya na ni ya mwisho kabisa kwa Hussein Machozi, namaanisha naacha muziki, naacha Bongo fleva nakuwa mtu wa kawaida raia wa kawaida ambaye nitaishi maisha yangu ya kawaida.” Amesema Hussein.
Ametoa sababu za kuchukua uamuzi huo mgumu kwake.
“ Sababu ni kwamba kuna kitu ambacho kikubwa nakifanya kwenye maisha yangu ambacho kitanibadilishia maisha yangu kiurahisi kwasababu ninakimudu kufanya,” alieleza.
“Nasikia vibaya sana na inaniuma sana kuwaacha Watanzania kwa style kama hii, ukiangalia kwa hali ya haraka haraka huwezi endelea kufanya kitu ambacho hakikuingizii kwa sasa hivi kwasababu masha yamebadilika, huwezi kuwa unafanya muziki tu unatoa muziki wenyewe hauingizi” alisema Hussein.
Hussin ameongeza kuwa wimbo mpya anatarajia kuuachia wiki mbili zijazo ni zawadi kwa mashabiki waliom-support kwa kipindi chote alichokuwa akiwaburudisha.
“Na pia nafanya hivyo kwasababau ya heshima ya Watanzania sipendi kuwaacha vibaya kwahiyo nimeamua kuwapa hiyo zawadi ambayo itatoka baada ya wiki mbili kwa heshima kwao kwasababu bado nina mapenzi kwao siwezi kuondoka tu hivi hivi ni bora niwaache na kitu ambacho angalau watakaa kumkumbuka Hussein Machozi alituachia kitu hiki wakati anaacha muziki.” Alimaliza Hussein Machozi.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.