Wema, Aunt Wakwepana Ikulu, Kisa ? Soma Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema, Aunt Wakwepana Ikulu, Kisa ? Soma Hapa

Bet Sasa
MAHASIMU wawili katika anga la mastaa, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wiki iliyopita walikwepana na kushindwa kusalimiana, licha ya wote kuwa waalikwa katika hafla maalum ya kujipongeza iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Gazeti hili ambalo pia lilikuwepo kwenye viwanja hivyo vilivyosheheni mastaa wa fani mbalimbali, liliwaona wawili hao ambao awali walikuwa marafiki wakubwa, wakijivinjari kwa tahadhari ili wasikutane, licha ya nyakati tofauti kuzungumza na mastaa wengine.
Aunt Ezekiel ambaye wakati wa kampeni hizo alikuwa kundi lililopewa jina la Nimestuka, naye alijichanganya na waalikwa wengine lakini jicho lake likiwa makini kuhakikisha hakutani hata sehemu moja na muigizaji huyo wa Filamu ya Madam.
Katika sherehe hiyo pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa kitaifa wa serikali iliyopita, akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mkewe, mama Salma Kikwete na waziri mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga na mkewe.
Mastaa wengine waliojumuika katika hafla hiyo iliyochagizwa na muziki kutoka kwa Yamoto Band ni pamoja na mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi, Ally Choki, muigizaji mkongwe, Bi Mwenda, mlezi wa wasanii Mama Loraa na Emmanuel Mbasha.

Chanzo- GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.