Watanzania Wenzangu Tumombee Rais Wetu Kutokana na Hizi Changamoto Kubwa Kwake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Watanzania Wenzangu Tumombee Rais Wetu Kutokana na Hizi Changamoto Kubwa Kwake

Ninawaomba watanzania tumwombee Rais wet mheshimiwa Magufuli kutokana na changamoto zilizo mbele yake. Ninajua Magufuli ana moyo wa dhati kuwatumikia watanzania lakini yafuatayo ni changamoto kubwa kwake.

'1. Chama chake. Chama chake ni mzigo na yeye si mwenyekiti. Lolote akaloamua chama kinaweza kukataa na hawezi kufanya chochote. Kwa jinsi hii mabadiliko ya Magufuli ni ndoto, Hayo yatamshosha Magufuli upesi sana.

2. UKAWA. Kwa hali halisi Ukawa wana wanachama wengi sana na mpaka kesho wanaamini Lowassa ndiye rais Hii ni changamoto kufanya na watu wasiokukubali. Itabidi utumie nguvu kubwa sana kuwatawala.

3. Uchaguzi wa Zanzibar. Ninafikiri mambo ya Zanzibar yanamuumiza kichwa kama yanavyotuumiza na sisi

4. Kutekeleza ahadi zako ambazo kwa uhalisia wa chama chako hazitekelezi.

Kutokana na haya mambo ninaona utawala wa Magufuli ukiwa mgumu kwa wakati huu wa mwanzo ndiyo maana watu wanaotakia nchi yetu mema inabidi tumombee hili Mungu ampe hekima katika kukabiliana nayo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.