Trey Songz kufanya show nyingine Afrika mwezi December - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Trey Songz kufanya show nyingine Afrika mwezi December

Mwimbaji wa RnB, Trey Songz kutoka Marekani anakuja tena Afrika, lakini safari hii anaenda Lagos, Nigeria ambako amethibitishwa kuwa atatumbuiza mwezi December katika tamasha kubwa la Rhythm Unplugged.
Trey Songz
Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka hukutanisha wasanii karibu wote wa A-List wa Nigeria, pamoja na msanii mmoja mkubwa kutoka nje. Mwaka huu litafanyika Ijumaa ya December 18.
Kwa mwaka huu, hii itakuwa ni mara ya pili kwa Trey Songz kufanya show Afrika, baada ya kutumbuiza Durban na Johannessburg, Afrika Kusini mwezi August.
Mwimbaji Kutoka Tanzania Vanessa Mdee a.k.a Vee Money pia aliwahi kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo mwaka 2013. Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.