Shilole Atoboa Sababu ya Kuuza Nyumba Yake Aliyokua Anajenga Kimara - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole Atoboa Sababu ya Kuuza Nyumba Yake Aliyokua Anajenga Kimara

Msanii Shilole aliwai kuingia kwenye headlines baada ya ku-post kwenye instagram picha ya nyumba yake ambayo alikua bado anaijenga. Caption ya picha hiyo ilikua inasomeka hivi, “Mungu nisaidie nimalize hii kitu ili watoto wangu wasije kupata tabu”.
Eneo ambalo alilokua anajenga nyumba hiyo ni Kimara jijini Dar es Salaam lakini Shilole amesema kwamba ameuza nyumba hiyo ambayo ilikua bado haijaisha vizuri.
Akiongea na millardayo.com Shilole ametoa sababu za kuuza nyumba hiyo kama hivi, “Nyumba yangu niliyokua naijenga maeneo ya Kimara nimeiuza kwenye hatua iliyofikia kama ilivyokua inaonekana kwenye picha. Sababu ya msingi iliyonifanya kuiuza ni kwamba pale eneo nililokua najenga ni nimegundua kwamba ni njia ya maji. Hivyo basi sitaki kupata tabu msimu wa mvua ukianza maji yakiwa yanapita nje ya nyumba yangu. Pia hakuna tatizo nimeuza nitajenga kwingine mambo ni mazuri”
Millardayo.Com

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.