Prof. Mwangamila Aliondoka na Amina Sanani Ametangulia ni Uamuzi wa Allah. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Prof. Mwangamila Aliondoka na Amina Sanani Ametangulia ni Uamuzi wa Allah.


Mwandishi Kiduo Mgunga

Ni miezi imepita tangu Prof.Mwangamila atangulie mbele za haki.Ulikuwa wakati mgumu sana  

na ilichukua muda huzuni kunitoka ila kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti kifo chake kitabaki 

kuwa  mazingatio na kunikumbusha kuwa safari yetu ni mmoja.

Nikiwa bado namkumbuka Mwangamila rafiki yangu wa kubadilishana mawazo na mijadala 

mipana yenye tija ya kujifunza kila kukicha.Nilimkumbuka zaidi siku ya mahafali (2015) na 

nilimkumbuka zaidi Amina Sanani wote walinipa uzuni kwa kiwango tofauti,ilinipa wakati 

mgumu kujiona nipo katika sherehe yangu muhimu.

Siku zikapita baaada ya mahafali lakini Ilipofika Jumatano niliuliza Amina  anaendeleaje 

niliambiwa anaendelea vizuri na ametoka Dodoma yuko Bagamoyo nikaomba zitafutwe taarifa 

zaidi kuhusu hali yake z kisha nikasisitiza tuendele kumuombea mwezetu.

Lakini sikujua kuwa nyakati zinakalibia na hata kuwa pamoja nasi.Nakumbuka Ilipofika 

Alhamisi taarifa ikatolewa kuwa Amina hayupo tena nasi.Mwili ulinyongonyea na moyo uliumia 

lakini nikajisemea “Kwa Allah sote tutalejea’’.

Nilikumbuka mambo mengi  muhimu leo nitasema machache na mengine nitaeleza siku za 

usoni.Nakumbuka Amina alipenda sana kutumia nukuu hii ‘’Girl live by dreams’’ kisha 

nikajisemea amejitaidi sana kufikia ndoto zake kama kijana lakini leo ameondoka.Sisi tuliobaki 

lazima tujifunze kuwa na ndoto ili tukiondoka tuache mawazo ya ndoto zetu au tuache ndoto 

iliyotekelezeka kwa faida yetu na wengine.Amina alijua umuhimu wa ndoto na aliamua 

kushikilia kauli mbiu yake kwa dhati kabisa.

Nakumbuka 2012 nikiwa mwaka kwanza  tulikuwa na jukumu la kuwasilisha mada na 

kuhakikisha wanafunzi wenzetu wanapata hamasa ya kuchangia mjadala  na kuelewa mada hiyo 

kwa upana wake.Ilikuwa katika somo la ‘’Genera Studies’’ na somo hili lilijumuisha wanafunzi 

kutoka fakati mbalimbali na mawazo tofauti yalikutana kisha kupambana na kusuguana kwa 

kiwango cha juu zaidi.

Nakumbuka wanafunzi walikuwa wengi na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwasilisha mada 

mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu na nilijianda vizuri ili kuhakikisha naweka rekodi sawa na 

heshima kama mtaji wa siku za usoni.

Nakumbuka mimi nilikuwa mzungumzaji wa tatu na nilijitaidi kuwa na mifano mingi na 

maelezo mazuri.Baada ya mimi na wanafunzi wenzangu kumaliza uwasilishaji wa 

mada,wanafunzi wenzetu walitupongeza  kisha  Mhadiri  alihitimisha mjadala.

Nakumbuka jambo mmoja muhimu baada ya mnyukano ule wa mawazo alitokea mtu mmoja tuu 

aliyeniambia  ‘’Congratution you did it’’ maneno haya machache yamenijenga sana na 

nilijifunza  tabia ya kuwapa wengine moyo wa kujituma zaidi na limenipa hamasa zaidi kila 

nikiajanda kujadili mada na limenisaidia kupenda kujisomea zaidi ili katika mijadala niendele 

kuwa bora zaidi.Nitakumbuka sana mchango huu uliotukuka wa maneno mchache uuliosemwa 

na Amina Sanani.

Ilipofika mwaka 2015 nilipoamua kugombea Ubunge na kuwaeleza wanafunzi wenzangu Amina 

alikuwa mtu wa kwanza kupenda kunitania Mhe.Mbunge, kwangu ilikuwa faraja kubwa kwa 

kupata hamasa yake ya kuonyesha kuwa mpango wa kugombea utafanikiwa.Nilipopitisha 

karatasi ya mchango Amina alikuwa mmoja wa watu walionichangi kwa maneno machache 

napenda niseme alitoa baraka zote na hamasa katika moyo wangu ya kuendelea kusonga mbele.

 Japo siku fani kiwa kuwa mgombea lakini niliweza kujenga msingi wa safari ya kuwa tumikia 

wananchi siku za usoni.Najua kwa uwezo wa Allah siku mmoja nitafanikisha lengo la kuwa 

tumikia wananchi.Japo Amina ametangulia lakini ameniacha na mchango mkubwa katika safari 

yangu ya kisiasa.

Jambo la mwisho ambalo nitalikumbuka sana,hadi namiliza chuo kuna watu watano ambao 

nimebadilishana nao sana mawazo na tumekuwa marafiki wakaribu sana lakini hadi sasa wawili 

wametangulia mbele za haki (Prof.Mwangamila na Amina Sanani) watu hawa kila mmoja 

alikuwa na sifa zake lakini kwa muda mfupi sana niliweza kujifunza mengi kutoka kwao na wao 

walijifunza mengi kutoka kwangu na naona ni jukumu langu kuangali  mawazo walio kuwa 

wanafanana na yale waliotofautiani kwa namna gani nawweza kutekeleza ili ya saidie kizaizi cha 

leo na kijacho. 

Prof.Mwangamila  na Amina Sanani pumzikeni kwa Amani.Bado nakumbuka mawazo yenu 

muhimu na dunia itajifunza mengi kutoka kwenu ikiwa nitafanikisha kuelimisha, kujadili, 

kutekeleza na kusimamia mawazo yenu.Allah akipenda nitatimiza na tutakuwa pamoja siku 

mmoja.

Napenda ni hitimishe kwa kusema najivunia na kufurahi kujifunza kutoka kwa watu hawa 

wawili Prof. Mwangamila na Amina Sanani.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.