Nipo Vizuri Sina Tatizo la Uzazi – asema Linah na Kukanusha Kuwa Sio Mjamzito - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nipo Vizuri Sina Tatizo la Uzazi – asema Linah na Kukanusha Kuwa Sio Mjamzito

Linah Sanga amekanusha uvumi kuwa ana ujauzito na kuweka taarifa sawa kuhusu afya yake ya uzazi.
Linah
Mwimbaji huyo wa ‘No Stress’ amesema kuwa kwasasa anajipanga ndio maana hajaamua kupata mtoto lakini hiyo haimaanishi kuwa ana matatizo yoyote ya uzazi kama baadhi ya watu wanavyohisi.
“Mimi nipo vizuri bhanaa sina tatizo la uzazi ila huwa najipanga ndio maana watu hawajahi kuniona nina ujauzito, lakini kwa sasa najiachia sanaa hivyo muda wowote wanaweza kusikia jambo,” alisema Linah kupitia Planet Bongo ya EATV.
Hii si mara ya kwanza Linah kukanusha taarifa za kuwa mjamzito. Mwaka jana (2014) mwanzoni Linah aliwahi kukanusha taarifa kama hizo, na kusema maswala ya ujauzito, kuolewa na kuwa na familia ni ya muhimu kwa kila msichana lakini upande wake muda wa kuvifanya hivyo ulikuwa bado.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.