Nay Wa Mitego Aja Na Hii "Nitaimba Hata Taarab Kama Inalipa" Soma Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay Wa Mitego Aja Na Hii "Nitaimba Hata Taarab Kama Inalipa" Soma Hapa

Baada ya kutoa wimbo mpya, Nyumbani Kwetu, Nay wa Mitego amedai kuwa amepokea changamoto za baadhi ya wasanii kumdiss kuwa amehama kwenye hip hop na kufanya muziki mwingine.

Nay ameiambia Bongo5 kuwa anafanya muziki unaohitajika na mashabiki wake na yupo tayari kuimba hata Taarab kama itamlipa.
“Wapo ambao wanaendelea kudiss nimetoka kabisa kwenye Hip Hop na sipaswi kujiita mwanahiphop. Muziki ndio kazi yangu na ninafanya kile wanachohitaji mashabiki, nitaimba hata Taarab kama itakuwa inalipa,” amesema Nay.
“Mimi hata wakidiss, kwangu ni furaha tu. Mimi ninachoangalia ni hela. Ni mwanamuziki mfanyabiashara, muziki ninaoupenda ni hip hop na ninaufanya hata kuliko wanavyofanya wao. Nikifanya huu pia nafanya kuliko hata hao wanaofanya. Mimi naangalia mashabiki wangu wanataka nini. Wanadiss wakati wanasikiliza nyimbo zangu ndio maana wanapata nafasi ya kudiss.”

-Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.