Kigogo Atenga 10m Kumnasa Mrembo Kidoa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kigogo Atenga 10m Kumnasa Mrembo Kidoa

FEDHA inaongea! Kigogo mmoja aliyeomba jina lake lihifadhiwe, amedaiwa ‘kukolea’ kimahaba kwa Video Queen mwenye mvuto wa aina yake, Asha Salumu ‘Kidoa’ kiasi cha kutangaza dau la shilingi milioni kumi.
Chanzo chetu makini kilicho beneti na kigogo huyo anayemiliki yadi kadhaa za magari hapa Bongo, kimesema bosi huyo kila wakati amekuwa akimzungumzia Kidoa na kuahidi kumpa shilingi milioni kumi endapo tu atafanikiwa kulipata penzi lake.
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi na kusema kwamba kigogo huyo amekuwa akihaha kila kona kutafuta namba za simu za Kidoa ili aweze kuzungumza naye na kuelewana na hatimaye kumpa malavidavi.

“Jamaa yangu amechanganyikiwa mno, hatulii, kila wakati anamuulizia Kidoa huku akiahidi kumpatia milioni kumi kama tu atafanikiwa japo kuwa naye usiku kucha kwani kama mademu kaona wengi, ila kwa Kidoa, moyo wake umegota kabisa. Kila siku anahaha kutafuta namba yake, hajaipata ila yupo radhi kuinunua kwa gharama yoyote ile,” kilisema chanzo hicho.
Mara baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alimvutia waya kigogo huyo ambapo alikiri kumsaka mrembo huyo kwa hali na mali lakini akaomba asiandikwe gazetini.
“Jamani kama mnaweza mnisaidie. Mtoto kaumbika, nilianza kumuona kwenye ile video ya Akadumba ya Nay wa Mitego sasa picha zake zinazotoka katika magazeti zinanidatisha kweli nisaidieni ila ‘please’ msiniandike gazetini,” alisema kigogo huyo.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.