Kidoa Wa "Akadumba" Akomaa na Madairekta Wapenda Ngono - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kidoa Wa "Akadumba" Akomaa na Madairekta Wapenda Ngono

AshaSalumKidoa
VIDEO Queen wa Ngoma ya Akadumba, Asha Salum ‘Kidoa’ amewakomalia madairekta wa filamu Bongo wanaopenda ngono kisha watoe kazi kuwa hatakubaliananao kirahisi na kwamba kwake ni kazi tu.
Akipiga stori mbili-tatu na kona ya Bongo Movies, Kidoa ambaye kwa sasa ameingia katika filamu rasmi amesema kuwa, madairekta wengi Bongo wanaendekeza sana ngono ndiyo wampe mtu nafasi katika kucheza filamu jambo ambalo hatakubali limtokee.
“Nimekutana na madairekta wengi wanaoendekeza ngono kwenye kazi. Sasa nimeshaingia kwenye filamu hivyo madairekta uchwara wataisoma namba maana hapa kwangu ni kazi tu na si vinginevyo,” alisema Kidoa.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.