Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Kilichotokea Jana Wabunge wa Ukawa Kutoka Nje na yeye Kutokusimama Wakati Dk Shein Anaingia Bungeni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Kilichotokea Jana Wabunge wa Ukawa Kutoka Nje na yeye Kutokusimama Wakati Dk Shein Anaingia Bungeni

"Simtambui Dkt. Shein kama Rais wa Zanzibar Nataka tu kuweka rekodi sawa. Nilimpinga Dkt. Ali Mohamed Shein hadharani na jana bungeni. Alipoingia Shein bungeni sikusimama kama inavyotakiwa. Nilikaa chini kupinga uhalali wake. 
Alipoingia Rais John Magufuli nilisimama na kumpa heshima yake kama Rais na kukaa kumsikiliza. Kuendelea kuzomea wakati Rais halali kaingia Bungeni kuzindua Bunge ili wabunge waanze kazi ni kutokuwa na mikakati sahihi. Ilitosha kumzomea Shein na kukaa chini bila kusimama alipoingia kama tulivyofanya. Wenzangu hawakujua pa kuishia. 
Magufuli anapambana na rushwa. Mimi napambana na rushwa. Namwunga mkono katika vita dhidi ya rushwa. 
Anayempinga Magufuli kwa vyovyote vile anatetea wala rushwa na mafisadi. Anayempinga Magufuli ni yule anayeogopa viwanda na mashamba yaliyobinafsishwa kurudishwa Kwa umma".
-Zitto Z Kabwe

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.