JB ALISHWA SUMU ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

JB ALISHWA SUMU !

Habari mbaya iliyolifikia gazeti hili imeeleza kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Jacob Stephen ‘JB’ amenusurika kifo baada ya kudaiwa kulishwa sumu na kujikuta katika hali mbaya kiafya kabla ya kukimbizwa hospitalini.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa JB, masaibu hayo yalimkuta wikiendi iliyopita akiwa katika mishemishe zake kwenye viunga mbalimbali vya Jiji la Dar.
Inadaiwa JB alizidiwa Jumamosi iliyopita alipoanza kulalamika kukatwa na tumbo, lakini wenzake wakachukulia poa na kumshauri kwenda kuchukua vipimo hospitali.
“Baada ya vipimo alipewa dozi akarudi nyumbani lakini asubuhi yake (Jumapili), hali ilizidi kuwa mbaya zaidi ndipo akakimbizwa Hospitali ya Marie Stopes (Mwenge, Dar).
Gazeti hili lilifika Marie Stopes na kuzungumza na baadhi ya wauguzi ambao walikiri JB kufikishwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya.
“Madaktari waligundua kwamba alikuwa amelishwa sumu lakini mwenyewe alikuwa haelewi alichopewa kwa sababu alisema alikuwa amekula vitu mbalimbali tena sehemu tofauti,” alisema mmoja wa wauguzi hao ambaye aliomba hifadhi ya jina.
Akizungumza na gazeti hili kwa tabu, JB ambaye kwa muda mrefu alikuwa akizunguka mikoani kwenye kampeni za uchaguzi alisema kuwa alishangaa kujikuta akishindwa kuendelea na ratiba zake za kazi kufuatia kusumbuliwa na tumbo lililokuwa likimkata kabla ya kugundulika kuwa alilishwa chakula chenye sumu.
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri lakini hali ilikuwa mbaya mno, bado sijaweza kutoka ndani naendelea na dozi,” alisema JB akiomba aendelee kupumzika.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.