Diamond: Nyimbo na Video Ninazoenda Kuachia Mwaka Huu zitakuwa ni Historia Hadi Siku Ntapozikwa ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond: Nyimbo na Video Ninazoenda Kuachia Mwaka Huu zitakuwa ni Historia Hadi Siku Ntapozikwa !

Bet Sasa
Diamond ni miongoni mwa wasanii ambao waliahidi kuachia kazi mpya baada ya uchaguzi, na kati ya kazi alizofanya, inayosubiriwa kwa hamu zaidi ni wimbo aliomshirikisha staa wa RnB kutoka Marekani, Ne-Yo.
Mpaka sasa bado haijafahamika ni wimbo/nyimbo gani atakazotangulia kuachia, kutokana na style yake ya kufanya vitu kimya kimya mpaka dakika za mwisho akiwa na kila kitu mkononi ndio huwa anaanza kutoa ishara.
Platnumz juzi (Nov.9) aliandika post ambayo ni kama ishara ya kuwaandaa mashabiki wake wakae mkao wa kupokea kazi mpya.

Kwa kujiamini kupita maelezo, kupitia mitandao ya kijamii baba wa Tiffah aliandika;

Nyimbo na Videos nnazoenda kuachia mwaka huu, zitakuwa ni Historia na Kubaki kumbukumbu hadi siku ntapozikwa…. #HifadhiHiipost.” kwa maneno haya, hii ni ishara kuwa mzigo unadondoka muda si mrefu? Nadhani majibu tutayapata soon.

Nyimbo na Videos nnazoenda kuachia mwaka huu, zitakuwa ni Historia na Kubaki kumbukumbu hadi siku ntapozikwa…. #HifadhiHiipost

— Chibu Dangote (@diamondplatnumz) November 9, 2015

Kwa tafsiri ya kile alichoandika Diamond, “Nyimbo” na “VideoS”, hii inamaanisha tutarajie wimbo zaidi ya mmoja (1) , pamoja na video zaidi ya moja (1) ndani ya siku 51 zilizosailia kuumaliza mwaka huu wa 2015. #HifadhiHiipost

By-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.