Diamond na AKA washoot video ya collabo yao Afrika Kusini - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond na AKA washoot video ya collabo yao Afrika Kusini

Rapper Kiernan Jarryd Forbes, maarufu kama AKA na staa wetu Nasibu Abdul aka Diamond Platnumz wameingia location kushoot video ya collabo yao.
AKA X Diamond
Taarifa ya kufanyika kwa video hiyo imetolewa na AKA kupitia akaunti yake ya Twitter jana Jumapili.
Inavyoonekana video hiyo inashutiwa Afrika Kusini kwasababu Diamond Platnumz yuko huko toka wiki iliyopita.
AKA na Diamond walipata nafasi ya kuingia studio kufanya collabo mwezi May mwaka huu, wakati rapper huyo alipokuja Tanzania kwenye Zari All White Party kwa mwaliko wa Diamond.
Hii itakuwa ni collabo ya pili kwa AKA kufanya na msanii wa TZ pamoja na kushoot video, baada ya kushirikishwa na Joh Makini kwenye ‘Don’t Bother’ inayofanya vizuri kwenye media mbalimbali Afrika Kusini na sehemu nyingine za Afrika.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.