Barnaba Hajatoa Hata Senti Kumshirikisha Jose Chameleone ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Barnaba Hajatoa Hata Senti Kumshirikisha Jose Chameleone !

Tumekuwa tukisikia juu ya ugumu wa wasanii wakubwa kukubali kufanya collabo na wasanii ambao wako chini yao, hususani collabo zinazokuwa zinahusisha wasanii kutoka nchi tofauti, na wengine hutoza pesa nyingi kama malipo ya kushiriki kwenye collabo hizo.
chameleone and Barnaba
Baada ya wimbo mpya wa Barnaba ‘Nakutunza’ aliomshirikisha Jose Chameleone kutoka Jumatatu wiki hii, amezungumzia jinsi Chameleone alivyojitolea kumsaidia bila kumtoza chochote.
“Sijamlipa hata mia moja, hakuna gharama kubwa ambayo Jose amenitoza” Baranaba aliiambia Ayo TV.
barnabas
Barnaba ameongeza kuwa licha ya kuwa hii ilikuwa ndio mara ya kwanza kufanya kazi na Chameleone, lakini staa huyo ameahidi kumsupport hata kwenye gharama zingine pale watakapohitajika kushoot video ya wimbo huo.
“Hata video yangu ninayoshoot nje ya nchi Jose ni one of the people ambaye ameshiriki kutoa pesa nyingi, kachangia mwenyewe kiasi kikubwa, hatujafanya bado vitu vingine viko kwenye finalizing lakini Jose ameniahidi popote nitakapoenda kushoot ameniahidi atatoa flight yake yeye na timu yake kuja kuhudhuria kwenye video yangu, na sio video tu hata siku ntakayotaka kufanya exclusive ya video kwasababu nitafanya show hapa Dar ameniahidi kuja.” Alisema Barnaba.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.