Wastara Aonesha Mahaba Niue Live Hakuna Siri Tena - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wastara Aonesha Mahaba Niue Live Hakuna Siri Tena

Live! Hakuna siri tena kati ya staa wa Bongo Movies, Wastara Juma na Mtangazaji wa Kipindi cha Action and Cut kinachorushwa kupitia Televisheni ya Channel Ten, Bond Bin Sinan baada ya kuonesha mahaba niue kwa kulishana keki kwa staili ya njiwa kwenye ‘bethidei’ ya mwigizaji huyo.

Habari kutoka kwa shushushu wetu zilidadavua kwamba, mpango mzima ulijiri kwenye bonge la pati ya kuzaliwa kwa Wastara iliyochukua nafasi katika Hoteli ya Sun-Rise iliyopo Kigamboni jijini Dar.

Katika pati hiyo ya kimyakimya, Wastara aliwaalika baadhi ya ndugu na marafiki zake ambapo mtangazaji huyo alikuwa mgeni maalum.

Sosi wetu huyo alitanabaisha kuwa walipofika hotelini hapo, baada ya watu kuanza kupata vinywaji ulifika muda wa keki ambapo Wastara aliwalisha watoto wake na baadhi ya ndugu wa karibu kisha alimuita mtangazaji huyo na kulishana naye keki kwa staili hiyo iliyogeuka gumzo.

“Unajua wale ni wapenzi lakini siku zote hawajawahi kuweka wazi uhusiano wao hadharani lakini sasa naona Wastara ameamua kuweka kila kitu wazi,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kumegewa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na Wastara ambapo alifunguka kuwa wageni wote aliowaalika aliwalisha keki kwa staili hiyo kuonesha ni wapenzi wake wa kweli.

“Jamani wageni wangu wote niliowaalika niliwalisha kwa staili hiyo na hao ndiyo wapenzi wangu wa ukweli kwa sababu hata watoto wangu na dada zangu niliwalisha kwa mdomo pia,” alisema Wastara.

Chanzo: GPL
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.