Video ya Belle 9 ‘Shauri Zao’ Yatambulishwa Kwa Kara ya Kwanza Trace Urban, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video ya Belle 9 ‘Shauri Zao’ Yatambulishwa Kwa Kara ya Kwanza Trace Urban, Ipo Hapa

Ndoto za wasanii wengi wa Tanzania zinaendelea kutimia bila kujali ni kwa muda gani wamekuwa wakiota bila kufahamu ni lini ndoto hizo zitakuja kuwa kweli.
Belle 9 Trace
Belle 9 ana kila sababu ya kufurahia mafanikio mapya, kwasababu kwa mara ya kwanza video yake ya ‘Shauri Zao’ iliyotoka kwenye vituo vya nyumbani wiki kadhaa zilizopita, imetambulishwa na kituo cha Ufaransa, Trace Urban na kuwa ndio video yake ya kwanza kuchezwa na kituo hicho cha kimataifa.
Belle kupitia Instagram ameshare screenshots na kuandika;
“Much respect and big time appreciation for ur support , our utmost gratitude goes out to the whole trace network @trace_urban @tracenigeria”
Video ya ‘Shauri zao’ imeongozwa na Hanscana na imefanyika hapa hapa Tanzania, hii ikiwa ni ishara kuwa kama msanii akiwekeza na kazi ikasimamiwa vizuri kuna uwezekano video za watayarishaji wa nyumbani zikaeleweka kwenye vituo vingi vya kimataifa.


-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.