VIDEO: Rubani Anafariki Katikati ya Safari Ndege Ikiwa Angani...Kilichotokea ni Hiki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

VIDEO: Rubani Anafariki Katikati ya Safari Ndege Ikiwa Angani...Kilichotokea ni Hiki


Dharura inaweza kutokea popote na wakati wowote, unaweza kupata picha hofu utakayokuwa nayo ikitokea mko katikati ya safari kwenye Ndege angani alafu Rubani anafariki !!
Ndege ya American Airlines iliyokuwa imetoka Phoenix kwenda Boston Marekani imelazimika kutua kwa dharura Uwanja wa Syracuse, Hancock International Airport New York baada ya Rubani wa Ndege hiyo, Michael Johnston kufariki… Kifo chake ilikuwa ghafla tu ambapo baada ya hali yake kuwa mbaya alianza kupata huduma ya msaada kutoka kwa mmoja ya wahudumu wa Ndege lakini muda mfupi baadae akafariki.

Msemaji wa Shirika la Ndege la American Airlines amesema Ndege ilitua salama kwa sababu ndani alikuwemo pia Rubani msaidizi, na kilichosaidia pia ni Sheria inayolazimisha kila ndege kuwa na Marubani wawili ndani.

Rubani Michael Johnston ambaye amefariki kwenye Ndege hiyo.
Ndege ilikuwa na jumla ya Abiria 147, mpaka sasa sababu ya kifo chake haijafahamika japo mkewe anasema huenda Michael Johnston alifariki kwa tatizo la pressure.
Taarifa ya stori yenyewe iko pia kwenye kipande hiki cha Video


Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.