Sijaoa Kwasababu Sina Muda Wa Familia – Flavour - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sijaoa Kwasababu Sina Muda Wa Familia – Flavour

Bet Sasa
Licha ya kuwa ana mashabiki wengi wa kike na anafanya muziki unaowalenga zaidi mashabiki wa kike, staa wa Nigeria, Flavour N’abania hafikirii kuoa na ametoa sababu zake za kuendelea kuwa mwanachama wa chama cha mabachela.
flavour-7
Tumeshawasikia wasanii wengi akiwemo Davido wakitoa sababu za kwanini hawajafikiria kuoa, lakini sababu aliyoitoa Flavour mwenye umri wa miaka 31 ni kuwa hajaoa kwasababu hana muda wa kuwa na familia kwa sasa.
Akizungumza kwenye mahojiano exclusive na Myjoyonline, Flavour amesema “Ndoa ni kitu kikubwa hivyo hutakiwi kukosea kufanya maamuzi, hicho ndio kitu cha muhimu.”
Aliongeza kwa kusema “Kama unataka kuoa ilimradi kuoa basi itakuwa haina maana, hauitafsiri maana ya ndoa, na kwasababu ya aina ya kazi tunayofanya, hua nakaa nyumbani mara chache sana sasa nitapata wapi muda wa kukaa na familia yangu? Ndio maana ni ngumu sana.”
Staa huyo ambaye ameshirikishwa kwenye hit song ya Diamond ‘Nana’ ameendelea kusema kuwa kama angekuwa anafanya kazi tofauti kama ya benki au CEO wa kampuni ingekuwa rahisi zaidi kwake kupata muda wa kutengeneza familia.
“Kwa karibia miezi miwili sasa sijakanyaga nyumbani, sasa kama ningekuwa na mke nini kingetokea? Inamaanisha nisingeweza kwenda kazini, ningepaswa kuwafikiria wao kwasababu siwezi kuwaacha wenyewe kiasi hicho.” alisema Flavour.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.